MWANAMKE WA KIGHANA AKAMATWA NA KILO 10 ZA MADAWA YA KULEVYA AKITOKEA TANZANIA

0 comments


Mfanyabiashara mwanamke wa Kighana (pichani) amekamatwa na kilo 10 za Heroin wakati akitokea Tanzania. Mercy Agyeman Prempeh (36) amekamatwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kotoka wakati akitokea Tanzania. Polisi walimtaka mwanamke huyo kutambua mizigo yake uwanjani kutokana na sehemu aliyokuwa anatokea yaani Tanzania. 

Baada ya kuhojiwa na polisi alidai kuwa rafiki yake wa Kitanzania ndiye aliyempa mzigo huo ampelekee mtu asiyejulikana anayeishi katika jiji la Accra kwa ada ya Dola za Kighana 2,500. Amedai mwenye mzigo alitakiwa akutane nae hapo airpot na kumpatia kiasi hicho cha fedha lakini anaamini amengia mitini baada ya yeye kukamatwa.

JOHARI: HARUSI YA RAY NITAKUWA MWANDAAJI CHAKULA

0 comments

MKONGWE kwenye sanaa Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa endapo ikitokea mkurugenzi mwenzake, Vincent Kigos akaoa, yeye atajitolea kuwa mwandaaji wa chakula.
Mkongwe kwenye sanaa Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
Akizungumza na mwanahabari wetu mwishoni mwa wiki iliyopita, Johari alisema yeye na Ray ni watu wa karibu kwa kuwa wameiongoza kampuni yao kwa muda mrefu hivyo katika jambo muhimu kama la ndoa, lazima ajitoe kinaga ubaga kufanikisha.
Msanii wa Bongo Muvi, Vincent Kigosi 'Ray'.
“Yani hata kama ikitokea kesho mkasikia Ray anaoa ujue kabisa nitakuwa muandazi kuhakikisha madikodiko yanawafikia waalikwa kwa wakati muafaka,” alisema Johari ambaye mara zote amekuwa akikanusha kuwa uhusiano wa

T.I.D ft PROF JAY-RAHA (Official Video)

0 commentsAUDIO | Hisia ft Rich mavoko - IMEFIKA TIME | Download

0 comments
MRISHO MPOTO AVUNJA UKIMYA..!! AAMUA KUNUNUA GARI YA HESHIMA..!! TAZAMA HAPA PICHA

0 comments


BIFU ZITO: LULU, JACKLINE WOLPER NA MISS TANZANIA 2012 WAGEUKA PAKA NA PANYA,.. SOMA KISA UCHEKE

0 comments


E LIZABETH Michael ‘Lulu’ anayetesa katika filamu za Kibongo, yupo kwenye bifu zito na mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2012, Husna Maulid ambaye anadai amempora bwana’ke.
Habari zinaeleza bifu lao limefikia hatua ya
kuanikana waziwazi hadi kumwagiana matusi kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram lakini huondoa majibizano yao machafu kila baada ya muda mfupi.

Chanzo cha habari hizi kinapasha kuwa ugomvi wa Lulu na Husna ni juu ya mwanaume huyo ambaye anaishi jijini Arusha aliyetajwa kwa jina moja la Seki anayeelezwa kuwa na pesa za kutosha kusumbua mjini. “Hao wanamgombea jamaa fulani wa Arusha, anaitwa Seki, ana mawe (pesa) mbaya.


Lakini wa kwanza kuwa na Seki ni Husna na Lulu alijua, sema Husna na huyo jamaa walikuwa wanagombana na kumwagana mara kwa mara. Sijui sasa nini kilimfanya Lulu kwenda kutembea tena na huyo jamaa wakati anajua ni wa shoga yake, labda ni baada ya kujua wamemwagana,” kilipasha chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hizi, mwandishi wetu aliwatafuta Lulu na Husna kwa ajili ya kuthibitisha madai hayo. Lulu alikuwa wa kwanza kupatikana ambapo alisema: “Jamani mimi simjui kabisa Husna Maulid wala hata katika fikra zangu hayupo... yaani kifupi simjui.”

Husna alipopatikana na kuelezwa mkanda mzima, kwanza alishangaa Lulu kutomjua, akasema: “Hakuna mtu asiyejua kuwa Lulu kanipora mwanaume wangu. Lakini anajifanya mjanja, tutaoneshana tu. Anajidai sana, anajifanya wa mjini hanijui mimi, lakini mimi ni wa mjini zaidi yake.”

DIVA WA CLOUDS FM ACHIA WAZI KIFUA CHAKE...NI SHIDAAAAAAA

0 comments

Hakika Mtandao wa Insta unazidi kushika kasi kwa Umaarufu kwa wadada kujianika Maungo yao ya mwili. sasa Imekuwa ndio fasheni kwa akina dada kutupia picha za mitego katika acount zao hizo. Leo hii Diva Lovenes Love Mtangazaji wa Clouds Fm naye ameingia kwenye list ya watu hao kwa Kutupia Mtupio Huu..
 
Je kama mtangazaji ni maandili kwa mwandishi wa habari au mtangazaji kufanya hivu vya namna hii au ndio kupeana shavu katika utangazaji sina imani kama mtangazaji mwenye taaruma hii huwezi fanya hivu vya namna hii kama anavyofanya DIVA  anajidhalilisha na anadhalilisha mama zetu na dada zetu na kuidhalilisha kazi ya utangazaji.
CREDIT - SWAHILI NEWZ

MAELFU YA WATU WAKWAMA MAPEMA LEO KWENYE STAND KUBWA JIJIN DAR ES SALAAM UBUNGO.

0 comments


Mabasi yaendayo Dar es Salaam yakiwa yamezuiliwa katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu, Morogoro baada ya eneo la Ruvu mkoani Pwani kujaa maji. Picha na Juma Mtanda


Dar es Salaam. Uharibifu wa barabara uliotokana na mvua zinazoendelea kunyesha, umeendelea kuwatesa wakazi wa Dar es Salaam na mikoa mbalimbali nchini hasa baada ya mabasi ya
mikoani kuzuiwa kufanya safari zake jana.
Amri ya kuzuia mabasi hayo ilitolewa jana ikiagiza mabasi yote yasiondoke katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo hadi itakapotangazwa vinginevyo, kutokana na uharibifu wa Barabara za Kilwa, Morogoro na Bagamoyo ambako madaraja yamevunjika.
Dereva wa Basi la Adventure liendalo Kigoma, Joseph Luciano alisema walitangaziwa na Sumatra na trafiki kuwa wasubiri mpaka hapo watakapojulishwa kuondoka.
“Hatuwezi kuondoka mpaka Serikali itakapotangaza ili kuepuka faini ambayo wenzetu, wale wanaopakia nje, wametozwa,” aliongeza huku ikielezwa kuwa baadhi ya mabasi yalitozwa faini kwa kukiuka amri hiyo.
Abiria anayesafiri kwenda Kibondo, Kigoma, Lydia Lutakinikwa alisema: “Nilikuja kuchukua mzigo wa duka langu tangu Ijumaa na nimekuwa nikilala gesti. Nimeishiwa hela hivyo nalazimika kuendelea kuwapo kwenye hili basi kwa kuwa sina tena pesa ya kwenda kulipia malazi.”
Kondakta wa Basi la Taqwa liendalo Nairobi, Yahaya Maulid alisema wameruhusu kubadilishwa tiketi za abiria wao, kama walivyoelekezwa na mamlaka husika ili kutoa nafasi kwao kujipanga upya.
Mkuu wa Usalama Barabarani Ubungo, Inspekta wa Polisi, Yusuf Kamutta alisema zaidi ya mabasi 400 yameathiriwa na uamuzi huo... “Tumezuia mawakala wasitoe tiketi mpya kwa sababu abiria wa leo (jana) ndiyo wanaotarajiwa kusafiri kesho, hivyo wanaweza kuuza tiketi za kuanzia keshokutwa.”


Chanzo: Mwananchi

TAZAMA PICHA NA STORY ZA SAA 72 ZA MWISHO WA MAALIM GURUMO

0 commentsMwanamuziki Muhidini Maalim Gurumo akiwa mahututi katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Stori: Oscar Ndauka

MWANAMUZI nguli wa muziki wa dansi nchini, Muhidini Maalim Gurumo aliyefahamika pia kama kamanda na mashabiki wa muziki wa dansi, aliyeaga dunia Jumapili iliyopita katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar, alikutana na mateso ya kwa saa 72 za mwisho wake baada ya kulazwa akiwa taabani kwa siku tatu.


Mtoto wa marehemu anayejulikana kwa jina la Abdalah aliliambia gazeti hili kuwa siku mauti yalipomfika baba yake katika wodi namba sita Jengo la Mwaisela, alimtembelea na kumkuta akiwa katika hali nzuri na alipopewa chakula alikula, akashiba lakini cha ajabu alisema hatakula tena.
Kijana huyo alisema muda mfupi baadaye, hali ya baba yake ilibadilika, akaanza kupumua kwa shida ndipo alipozidiwa na baadaye kukata roho.

Maalim Gurumo akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kabla ya kufikwa na mauti.

Mzee Gurumo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa mapafu kwa muda mrefu na aliwahi kulazwa katika hospitali hiyo ya Muhimbili.

Baadhi ya watu waliomtembelea mzee Gurumo kwa nyakati tofauti akiwa hospitalini hapo ni pamoja na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alimuombea afya njema na akaruhusiwa kurudi nyumbani.

Mzee Gurumo akiimba wakati wa uhai wake.

Kifo chake kimeacha simanzi si tu kwa familia yake, bali kwa wadau wa muziki wa dansi kwani alikuwa mwalimu na kiongozi wa wanamuziki wengi ambao sasa wanatamba. Baada ya kustaafu muziki, Mzee aliwahi kupewa zawadi ya gari na msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ aina ya Toyota Funcargo.

Akizungumzia msiba huo, Kiongozi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki alisema wamempoteza mwalimu wa muziki asiyekuwa na choyo ya kuelimisha.

Mzee Gurumo akiwa na mkewe.

“Ni kama tumepoteza tochi tukiwa kwenye msitu mnene usiku wa manane,” alisema.
Naye msemaji wa Bendi ya Mlimani Park Ochestra (Sikinde Ngoma ya Ukae), Jimmy Chika alipozungumza na gazeti hili alisema mzee Gurumo aliwahi kuja kuwatembelea na kuimba mwezi mmoja uliopita katika Ukumbi wa DDC, Kariakoo jijini Dar.

“Alikuja kama mara tatu hivi ukumbini, naona alikuwa kama anatuaga kwa sababu alikuwa mwanzilishi wa bendi na mbunifu wa mtindo wa Sikinde, aliubuni Septemba, 1978,” alisema Chika.Mzee Kassim Mapili, mwanamuziki wa mkongwe, kwa upande wake alisema kifo cha Gurumo ni pengo kubwa ambalo haliwezi kuzibika na akafafanua kuwa ni mtu ambaye hakuwa mbinafsi.


Mzee Gurumo akiwa na CD yenye nyimbo zake.

Baadhi ya wanamuziki ambao amefanya nao kazi kwa karibu ambao sasa watakuwa wanamlilia mwalimu wao ni pamoja na Hassan Rehani Bitchuka, Said Mabela, Roman Mng’ande ‘Romario’ na wengine wengi.

Gurumo pia ameacha simanzi katika miji mbalimbali nchini kwa kuwa amewahi kutembelea kimuziki na alifanikiwa kujizolea mashabiki lukuki.

Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni msiba ulikuwa nyumbani kwake Mabibo, Dar huku taratibu za mazishi zikifanyika. Ameacha mjane na watoto wanne.

Mungu ailaze roho ya marehemu maali pema peponi. Amina.
-GPL

PICHA ZA SHOW ALIYO FANYA RAPPER @OCTOPIZZO NCHINI GERMANY HIZI HAPA.

0 comments

octop9

octop4
octop1
octop5
octop3
octop6
octop7
octop8

DOWNLOAD NEW HIT NISHER0_ON TOP.

0 comments
Photo: Upo tayari Kusikia Ngoma Yangu Mpya??? Baada ya #PAPER niliyo fanya last year... tarehe 14.4.14 Inakuja Ngoma Mpya inayoitwa #ON_TOP... 

written/produced/mixed/composed/performed By N��SHER

Kuskia  Ngoma zangu Nyinginezo ingia www.reverbnation.com/nisher

Stay tuned 14.4.14 #ON_TOP

DOWNLOAD HEREVIDEO HUYU NDIE MBUNGE KUTOKA KENYA ALIYE SHAMBULIWA NA MAJAMBAZI.

0 comments

KUNDI LA WEUSI LAENDA KUFANYA VIDEO NCHINI KENYA, SABABU YA KUTOFANYA NA DIRECTOR NISHER IKO HAPA

0 comments

Z Vile vipande vya video za Weusi zilizokuwa na title ya ‘OTEA’ ambazo zimekuwa zikiziruka kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii ya  kuanzia wiki iliyopita, tayari imefahamika kuwa ni ujio wa video ya single yao mpya ijulikana nayo kama "Gere".

Nikki wa Pili akiwa kama msemaji wa Weusi amesema kuwa wameshoot video ya ‘Gere’ Nairobi, Kenya siku chache zilizopita na director Enos Olik ambaye pia alifanya video ya nguli kuroka kule nchini kenya  Jaguar ijulikana nayo kama ‘Kioo’.

Hizi ni baadhi ya picha zao walizo achia weusi kwenye akaunti zao za kijamii

Pia niki wa pili alifunguka juu ya sababu ya wao kutofanya Video na Director Maarufu hapa bongo ajulikanaye kama Director Nisher

“Bahati mbaya Nisher alikuwa yuko caught up na mambo mengi na sisi tulikuwa na haraka so tukashindwa, kwasababu Arusha na Nairobi sio mbali tukavuka tu boda tu fasta.”

Nikki ameongeza kuwa video ya ‘Gere’ itatoka wiki ijayo.Weusi wamesema kabla video ya ‘Gere’ haijatoka wanataka kuifanyia biashara kwa yeyote anayetaka kuipata exclusive kwa siku tano kabla haijatoka rasmi iwe ni kampuni, blogs, au mtu binafsi.


“Hiyo ni biashara kwa mfano labda kampuni labda Voda au nani tunaweza tukawapa wakaweka kwenye page yao labda ya Facebook ikawa inapatikana pale tu”. aliongeza hivyo 

MTIZAME MTOTO WA 2FACE IDIBIA KUTOKA NIGERIA ALIVYOKUWA.

0 comments
Idibia girls

New Video Timaya Ft. Sean Paul - Bum Bum Remix [Explicit Video].

0 comments