OMMY DIMPOZ KUPIGA SHOW TABORA NDANI YA REDS MISS TABORA 2013

11:51 PM

Kipaza hiki kuwika Tabora na kuburudisha masikio ya WanaTabora wakati wa kilele cha shindano la REDDS MISS TABORA (si yakukosa)

"Tia saini mwanangu Tabora wanakusubiria kwa hamu" Mgalula
"Msanii wa muziki wa kizazi kipya aliye juu kwa sasa Ommy
Dimpoz (kwa poz) ambaye kwa karibu miezi mitatu amekuwa katika bara la Ulaya akifanya maonesho katika nchi tofauti zikiwemo England, Holland, Norway, Sweden na nyingi nyingine amethibitisha kuwa ataporomosha show kali mjiniTabora mnamo tarehe 31/05/2013 katika kusindikiza kinyang'anyiro cha kumsaka mrembo wa shindano la Redds Miss Tabora 2013. Pichani ni picha kadhaa za Ommy Dimpoz akisaini mkataba wa kufanya onesho hilo kubwa huku akishuhudiwa na mlezi wa kamati ya Miss Tabora 2013 Bw Mgalula Fundikira. Hatua hii itakuwa ni kukidhi matamanio ya muda mrefu ya mashabiki wa Ommy Dimpoz Tabora kumshuhudia msanii wao kipenzi kwa ukaribu zaidi siku hiyo ya tarehe31/05/2013 ambapo shoka litaungua mpini utabaki!
Kaa kwa ukaribu kisikupite kitu mwanaburudani wa Tabora, utashanweka na kufanya yote dhidi ya burudani lukuki zitakazoandaliwa siku ya shindano kuu...."
Mlezi wa Kamati na muandaaji mkubwa wa shindano hili Bw. Mgalula alikitibitishia chanzo hiki cha habari akiwa mjini Barcelona nchini Spain ambako msanii alidondosha saini yake. 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »